Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Taifa Stars yaigaragaza Madagascar

E R43VVXsBMbG6N Wachezaji wa Taifa Stars wakimpongeza Nyoni

Tue, 7 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa Mkapa hatoki mtu! ndivyo unavyoweza kusema baada ya Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars kuibuka na ushindi katika mchezo wake wa kuwania kufuzu Fainali za kombe la Dunia nchini Qatar 2022.

Stars imeibuka na ushindi wa magoli 3-2 dhidi ya Madagascar katika mchezo uliochezwa katika dimba la Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Stars iliyokuwa ya kwanza kupata magoli ya haraka haraka katika mchezo huo kwani dakika ya pili tu ya mchezo walipata goli kwa mkwaju wa penati lililowekwa wavuni na Erasto Nyoni.

Alikuwa ni Novatus Dismas aliewainua tena watanzania kwa goli lake maridadi la dakika ya 26'.

Madagascar walicharuka na kujikuta wanapata goli dakika ya 36' lililowekwa wavuni na Njiva Rakotoharimalala, kabla ya Thomas Fontaine kuongeza la pili dakika ya 45 na kufanya timu hizo kwenda nmapumziko zikiwa 2-2.

Kipindi cha pili kilianza kwa tahadhari kubwa huku kila timu ikisaka goli la ushindi lakini alikua ni kiungo Feisal Salum "Fei toto" aliewahakikishia Watanzania kuondoka na Pointi tatu baada ya kufunga goli la ushindi dakika ya 53' ya mchezo.

Mpaka dakika 90 zinakamilika, Tanzania 3 na Madagascar 2 hivyo kuifanya Tanzania kuongoza katika msimamo wa kundi J, wakiwa na pointi 4 sawa sawa na Benin waliopo nafasi ya pili, huku DR Congo akikamata nafasi ya tatu akiwa na Pointi 2 na Madagascar wakiburuza mkia.

Kila timu katika kundi hilo imeshacheza michezo miwili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live