Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Taifa Stars ya mafanikio inayoenda Ivory Coast, Golini Tupo tayari?

Taifa Stars Imetotaaa Taifa Stars ya mafanikio inayoenda Ivory Coast, Golini Tupo tayari?

Tue, 5 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zimesalia siku chache tu kabla ya michuano ya 34 ya kombe la mataifa Ya Afrika kutimua vumbi huko Ivory Coast.

Huu ndio wakati wa wachezaji kuamua kama watakuwa sehemu ya nyota kadhaa wateule ambao wataliwakilisha taifa la Tanzania kwenye michuano hii au kuwa mpenzi mtazamaji.

Juhudi ndio zitampeleka mchezaji kuwa sehemu ya michuano hii mikubwa kabisa ngazi ya taifa barani Afrika.

Tanzania inaenda kushiriki kwa Mara ya tatu katika historia,Ni jambo kubwa na la heshima kwa nchi ambayo ina muelekeo mzuri kwenye soka kwa sasa.

Ni wakati wa wachezaji kuvuja jasho ili wapate nafasi ya kuliwakilisha taifa kwenye michuano hii,

Michuano ina faida nyingi katika maisha ya mchezaji kwani Kupitia michuano hii unaweza ukapata ofa nyingi kubwa ndani na nje ya nchi.

Mchezaji ambaye atakuwa sehemu ya kikosi moja kwa moja atapanda thamani na kuingia kwenye vitabu vya kihistoria ambayo haitafutika kwenye vitabu.

Kila mchezaji ana haki ya kuitwa kwenye timu ya taifa lake endapo tu ataonyesha kiwango bora klabuni kwake.

Kila la kheri Timu ya taifa ni ya kila mtu,Juhudi ndio zinakufanya uwe sehemu ya wachache wa kwenda kuipeperusha bendera,siku zilizobaki ni nyingi kumshawishi mwalimu kukujumuisha kikosini kuelekea Afcon 2023.

Changamoto kwa Kocha Mkuu inaanzia golini kwake ambapo Imejidhihirisha wazi pindi anapokosekana Aishi Manula basi wengine Wengine Umekuwa Mtihani mkubwa sana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live