Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Taifa Stars warejea nchini, Rais Samia awapa neno

Taifa Stars Warejea Nchini, Rais Samia Awapa Neno Taifa Stars warejea nchini, Rais Samia awapa neno

Mon, 29 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, @gersonmsigwa ametoa neno la Rais Samia kwa niaba yake, akiwapa salamu wachezaji na benchi la ufundi la Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars wakati walipowasili usiku wa kuamkia leo kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.

Stars imetua nchini ikitokea Cote d’ivoire, ambako ilikuwa ikishiriki michuano ya Kombe la Mataifa Afrika, #AFCON2023 kabla ya safari yao haijakatishwa kwenye hatua ya makundi ikipambana na timu za Morocco, Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC).

Michuano ya AFCON bado inaendelea katika hatua ya 16 bora na unaishuhudia kupitia #AzamSports3HD (kwa Tanzania pekee).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live