Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Taifa Stars tizi limenoga

Stars Pic Data Taifa Stars tizi limenoga

Sat, 9 Jan 2021 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

TIMU ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imeendelea na mazoezi leo Jumatatu asubuhi kujiweka sawa na mashindano ya CHAN yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Januari 16 nchini Cameroon.

Mashindano hayo yanahusisha wachezaji wanaocheza kwenye ligi za ndani za mataifa husika.

Katika mazoezi yaliyofanyika kwenye viwanja vya Gymkana jijini Dar es Salaam, Stars wakiongozwa na kocha mkuu wa timu hiyo Ettiene Ndayiragije walianza kwa kunyoosha viungo kwa muda wa dakika tano, kisha kukimbia kwa kuzunguka duara.

Baada ya hapo Ettiene aliwagawa wachezaji makundi mawili yenye timu mbili ambapo walitengeneza duara kwa kila kundi na kuanza kucheza mpira kwa kukabana kitimu zoezi lilofanyika kwa dakika 10.

Mazoezi mengine yaliendelea ikiwemo kukimbia kwa kuzunguka uwanja, kukimbia na mpira kwa kasi, kucheza uwanja mzima mazoezi yaliyomalizika saa 3:00 asubuhi.

Wakati huo huo makipa Juma Kaseja na Aboutwalib Msheri walikua wakiendelea na programu yao maalumu chini ya kocha wa makipa.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz