Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Taifa Stars kupewa Mil. 10 goli la Mama

MWANAFA BUNGENI Taifa Stars kupewa Mil. 10 goli la Mama

Mon, 19 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Waziri wa utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma (Mwana FA) amesema kuwa ile zawadi ya Milioni 10 kwa Timu ya Taifa Tanzania 'Taifa Stars' kutoka kwa Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan itakabidhiwa Leo June 19, 2023 kwa Timu hiyo kufuatia ushindi wao wa bao 1-0 dhidi ya timu ya Niger katika mchezo wa kufuzu Fainali za Maitafa Afrika (AFCON) uliopigwa jana kwenye dimba la Benjamin Mkapa.

Naibu Waziri Mwinjuma ameyasema hayo leo Juni 19, 2023, Bungeni wakati wa kipindi cha maswali na majibu.

Mwinjuma alianza kwa kuipongeza Timu ya Taifa Stars kwa ushindi Bao 1-0 dhidi ya Timu ya Niger ambapo amesema ushindi huo ni njia moja wapo ya kuiwezesha Timu hiyo kuelekea katika michuano ya fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) ambazo zitafanyika mwakani Nchini Senegal.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live