Dar es Salaam. Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ itacheza mechi ya kirafiki na Rwanda Oktoba 14 siku nne kabla ya kuivaa Sudan katika mchezo wa kusaka kufuzu kwa fainali za CHAN2020 Cameroon.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) mchana huu inasema Taifa Stars imepata mechi ya kirafiki dhidi ya Rwanda 'The Amavubi' mchezo uliopangwa kufanyika Oktoba 14 jijini Kigali Rwanda.
Mchezo huo utakuwa ni mchezo wa kwanza kwa Stars wa kirafiki katika utawala wa makocha wawili tofauti tangu Mnigeria Emmanuel Amunike mpaka sasa kaimu kocha Mrundi Ettiene Ndayiragije haikuwahi kupata mchezo wa kirafiki.
Mapema kabla ya kutimuliwa Amunike aliwasilisha changamoto kubwa ya timu hiyo kukosa mechi za kujipima nguvu ambapo fursa hiyo imekuwa ikikwamisha makocha kuweza kuwapima wachezaji wao.
TFF imesema mchezo huo dhidi ya Rwanda utakuwa ni katika kalenda ya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA).
Aidha TFF imethibitisha kuwa mchezo wa kikosi cha timu hiyo kwa wachezaji wa ndani kuwania kucheza Fainali cha CHAN sasa utapigwa jijini Omdurman katika Uwanja wa El Merreikh.
Pia Soma
- Jinsi marafiki wa Kashoggi walivyomkumbuka
- Zahera apangua idara zote Yanga ikivaa Polisi
- Niyonzima aanza na kombe Rwanda
Waamuzi hao watakuwa ni Thierry Nkuruzinza atakayekuwa mwamuzi wa kati akisaidiwa na mwamuzi msaidizi wa kwanza Willy Habimana na mwamuzi wa pili msaidizi akiwa Shabani Niyungeko wakati mwamuzi wa akiba akiwa Georges Gatogato