Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Taifa Stars kujiuliza mbele ya Niger, kufuzu AFCON

Stars Pic Taifa stars itacheza mchezo wa kwanza kesho dhidi ya Niger kuwania kufuzu fainali za AFCON 2023

Fri, 3 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars kitaanza safari ya kuwania tiketi ya kufuzu fainali za soka za mataifa barani Afrika AFCON zitakazofanyika nchini Ivory Coast mwakani 2023. Hapo kesho ambapo watacheza dhidi ya Niger ukiwa ni mchezo wa kundi F.

Taifa Stars imepangwa kundi F kwenye michezo ya kufuzu AFCON sambamba na timu za taifa za Algeria, Niger na Uganda. Ambapo timu mbili za juu kwenye kundi hili zitafuzu kucheza fainali hizo.

Kikosi cha Tanzani chini ya kocha Mkuu Kim Poulsen tayari kipo nchini Benini tayari kwa mchezo dhidi ya timu ya taifa ya Niger mchezo utakao chezwa kesho majira ya Saa 1:00 Usiku.

Stars inaingia kwenye mchezo huu ikiwa imeshinda mchezo mmoja tu kwenye michezo 5 ya mwisho, wameshinda michezo 2 na wametoka sare michezo miwili. Huu pia ni mchezo wa kihistoria kwani ni kwa mara ya kwanza timu hizi zinakuta kwenye mchezo wa kimashindano.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live