Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Taifa Stars inelekea AFCON 20225, hatima ya Manula haijulikani - Mchambuzi

Manulasz Hatima ya Manula haijulikani

Fri, 9 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwishoni mwa mwezi Agosti, wachezaji mbalimbali wa Kiafrika watakuwa wataripoti kambini kwa ajili ya raundi mbili za mechi za kufuzu Afcon 2025 inayokwenda kuchezwa Morocco.

Timu 4 za Tanzania zinazoshiriki michuano ya kimataifa Yanga, Azam, Simba na Coastal Union zote zinategemea kuingia kwenye michuano yake husika (Champions League, AFL na Confederations Cup) zote zina makipa wa Kigeni, Simba na Azam zina makipa wawili wageni, Yanga na Coastal Union zina kipa mmoja mgeni.

Mtanzania ambaye amekua kipa namba moja Taifa Stars hivi karibuni Aishi Manula future yake kwa msimu huu bado haijulikani.

Kipa aliyedaka Taifa Stars mechi ya mwisho ya kiushindani si kipa namba moja Kwa Klabu yake na kama makipa wote wageni wakiwa fit anakua kipa namna tatu.

Hii inamaanisha kuwa Mechi za kufuzu Afcon ijayo watcheza makipa ambao hawana nafasi za kuanza kwenye klabu zao.

Zaidi ya hapo,Yanga,Azam,Simba kote kuna makipa waliosign long term deals ambao si Wazawa,Swali langu ni moja.

Je, Tunaendaje kwenye Afcon ya 2027 au huu mjadala nimeuleta mapema sana?

Anaandika mchambuzi wa soka, Geof Lea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: