Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Taifa Stars iliwahi kuwatungua Morocco bao 3

Samatta Kiembaa Taifa Stars iliwahi kuwatungua Morocco bao 3

Tue, 21 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mara ya mwisho Tanzania tulicheza na Morocco katika uwanja wa Benjamin Mkapa wakati huo ukiitwa Uwanja wa Taifa ilikuwa tarehe 24/03/2013 ulikuwa ni mchezo wa kuwania kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia 2014 nikiwa sehemu ya kikosi hicho tulipata ushindi wa goli 3-1.

Magoli ya mchezo huo mawili yalifungwa na Mbwana Samatta dakika ya 67 na 80 huku goli la kwanza likifungwa na Thomas Ulimwengu dakika ya 46 kwa upande wa Morocco walipata goli la kufutia machozi kupitia kwa El Arabi dakika ya 90+3’.

Kwa bahati mbaya katika Kundi C lilikuwa na timu za Ivory Coast, Morocco, Gambia na sisi, hapo kigogo aliyeongoza Kundi alikuwa Ivory Coast alimaliza na alama 14, Morocco nafasi ya pili akiwa na alama 9 na Gambia akimaliza wa mwisho kwakuwa na alama 4.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live