Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Taifa Stars, Madagascar kupigwa bila mashabiki

Starz Kikosi cha Timu ya Taifa kikifanya mazoezi kujiwinda dhidi ya Madagascar

Mon, 6 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars kesho Septemba 7, itashuka dimbani katika Uwanja wa Mkapa Majira ya saa 10 jioni kupambana na Timu ya Madagascar ikiwa ni mchezo ya kuwania kufuzu kwa michuano mikubwa duniani ya Kombe la Dunia kule Qatar 2022.

Sasa shirikisho la Soka nchini TFF, kupitia kwa Afisa habari wake Clifford Ndimbo, amesema mchezo wa kesho hautakuwa na Mashabiki kutokana na Shirikisho la Soka Duniani FIFA kutoruhusu mashabiki ikiwa ni jitihada za kupambana na Janga la Covid-19.

Ndimbo amesema bado wanaendelea na mazungumzo kuona ni namna gani watafanaya ili mashabiki waruhusiwe lakini kwa mechi ya kesho hakutakuwa na Mashabiki.

Aidha Ndimbo amewataka watanzania popote pale walipo waishangilie Timu yao kwa kuwa sapoti yao ndio kitu cha msingi kwa sasa.

Hii ni mechi ya pili kwa Taifa Stars baada ya kutoa sare katika mechi ya kwanza dhidi ya DR Congo mapema mwezi huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live