Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Taifa Stars, Kenya vinara wa rafu

65549 Stars+pic

Fri, 5 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mbali na kuondolewa mapema kwenye Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) zinazoendelea huko Misri, timu za taifa za Tanzania ‘Taifa Stars’ na Kenya ‘Harambee Stars’ zimemaliza hatua ya makundi zikiwa zinaongoza kwa kupata idadi kubwa ya kadi katika mashindano hayo kuliko nyingine.

Harambee Stars ina kadi 10 tisa za njano na moja nyekundu, zikienda kwa Philemon Otieno, Ayub Masika, Joseph Okumu, Johanna Omolo, Victor Wanyama, Patrick Matasi na Aboud Omar.

Tanzania inashika nafasi ya pili ikiwa na kadi saba za njano zilizotolewa kwa wachezaji Himid Mao, Mudathir Yahya, Feisal Salum, Saimon Msuva, David Mwantika, Hassan Kessy na Adi Yussuf.

Katika kundi hilo la timu zinazoongoza kwa kupata idadi kubwa ya kadi, nyuma ya Tanzania kuna Mauritania, Burundi na DR Congo ambazo nazo zimepata jumla ya kadi saba za njano kwenye hatua hiyo ya makundi.

Hadi hatua ya makundi inamalizika ni wachezaji watatu tu ambao wameonja kadi nyekundu ambao ni Philemon Otieno wa Kenya, John Boye wa Ghana na Nduwarugira Christophe wa Burundi.

Otieno anaongoza kupata idadi kubwa tatu za njano na moja nyekundu Ghilane Chaalali (Tunisia), Merveille Bokadi (DR Congo), Kasim Adams (Ghana), Themba Zwane (Afrika Kusini), Steve Mounie (Benin), Marco Ilaimaharitra (Madagascar), Deon Hotto (Namibia) na Bruno Gaspar (Angola) ambao kila mmoja ameonyeshwa kadi mbili za njano.

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz