Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Taifa Stars: Bado hatujamaliza kazi

Taifa Stars Amuhq.jpeg Taifa Stars: Bado hatujamaliza kazi

Wed, 11 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msaidizi wa Taifa Stars, Juma Mgunda amesema kazi bado haijasha, hivyo hawapaswi kubweteka, zaidi ni kujipanga na michezo miwili ijayo dhidi ya DR Congo.

Mgunda amesema hayo baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Guinea jana nchini Ivory Coast, huku akiweka msisitizo kuwa bado wapo kwenye marathon wanatakiwa kuelekeza nguvu zao katika michezo ijayo.

Amesema: “Tunawashukuru vijana kwa kujituma na kuonesha juhudi lakini nieleze kuwa hii ni marathon tuna kazi kubwa mbele, tutapumzika kidogo kisha tutarudi kujiandaa na michezo miwili ijayo.”

Stars imefika pointi nne nyuma ya kinara DR Congo mwenye pointi sita katika Kundi H kuwania nafasi ya kufuzu fainali za Afrika zitakazofanyika Morocco mwaka 2025.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live