Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Taifa Queens yapoteza mechi ya pili Afrika

Ac26fc4f4f3727c7514d04bb28e7d2b9 Taifa Queens yapoteza mechi ya pili Afrika

Wed, 10 Nov 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Timu ya taifa ya netiboli (Taifa Queens) imepoteza mchezo wake wa pili kwenye mashindano ya mataifa ya Afrika yanayoendelea nchini Namibia.

Queens imeruhusu kipigo cha magoli 55- 34 dhidi ya Zambia moja ya timu bora za Afrika.

Katika mchezo huo uliomalizika dakika chache zilizopita mjini Windhoek,  Queens ilionekana kuzidiwa uzoefu na mara kadhaa ilipoteza mipira kwa kufanya contact na steping.

Kingine kilichowagharimu Queens ni kutofunguka wanapokuwa na mpira hivyo kuwalazimisha kuchelewa kutoa pasi na kuwapa wapinzani wao nafasi ya kuwanyang'anya mpira.

Queens ambayo ilikuwa ya kwanza kupewa 'center pass' ilishindwa kuanza vema mchezo huo kwa kunyanganywa mpira na Zambia kufunga.

Mfungaji wa Queens, Mwanaidi Hassan licha ya kuwa mrefu zaidi ya GK wa Zambia, lakini alikutana na wakati mgumu kutoka kwa mzuiaji huyo ambaye alikuwa mahiri kwa kuruka na mara kadhaa alipangua pasi za mwisho ambazo zilitoka kwa center, winger attack na goal attack wa Tanzania kuelekezwa kwa mfungaji.

Hiyo ni mechi ya pili kwa Queens kupoteza kwenye mashindano hayo baada ya jana kuchapwa na She Cranes ya Uganda ambayo pia ni miongoni mwa timu zenye rekodi ya juu Afrika kama ilivyo kwa Zambia.

Hata hivyo, Queens imeshiriki mashindano hayo ikiwa ni mara ya kwanza tangu iliposhiriki mara ya mwisho mwaka 2012 na kuwa bingwa, Tanzania ikiwa mwenyeji.

Kuanzia mwaka 2014 timu hiyo haikuwa kushiriki mashindano hayo na kujikuta ikiporomoka kwenye renki kutoka nafasi ya tatu hadi kuondolewa kabisa.

Mwenyekiti wa Chaneta, Dk Devotha Marwa amesema hata kama watamaliza katika nafasi ya 40, lakini matamanio yao ni kurudi kwenye renki ya kimataifa, ambayo mashindano hayo yatakayofikia tamati Novemba 15 yatawapa nafasi ya kurejea upya kwenye viwango vya kimataifa.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz