Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tabora Utd kamili kuivaa Singida FG

Image 222 1024x640.png Tabora Utd kamili kuivaa Singida FG

Mon, 21 Aug 2023 Chanzo: Dar24

Uongozi wa Tabora United (Kitayosce FC), umesema tayari wameshughulikia suala la wachezaji wao wa kimataifa na sasa watakuwapo kwenye mchezo wa pili Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Singida Fountain Gate FC utakaopigwa Agosti 31, mwaka huu.

Katika mechi ya kwanza ya ligi hiyo, Tabora United walishindwa kutumia wachezaji wao wakigeni akiwamo Papy Tshishimbi aliyewahi kuichezea Young Africans, nyota wengine ni Andy Bikoko kutoka DR Congo, Toauya Jean (Burundi) na Mkongomani Lumiere Banza aliyekuwa akiichezea TP Mazembe.

Meneja wa timu hiyo, Rashid Hassan, amesema baada ya kutokea sintofahamu kwa kuwakosa wachezaji wao wa kigeni katika mchezo dhidi ya Azam FC kutokana na majina yao kutokuwapo kwenye mfumo rasmi wa usajili, lakini kwa sasa tayari wameshafanyia kazi tatizo hilo na mechi dhidi ya Singida Fountain Gate FC watakuwa miongoni mwa watakaounda kikosi cha timu hiyo.

Amesema kulikuwa na changmoto ya kiuongozi na ameshafanyia kazi na tayari wachezaji na timu hiyo wameweka kambi Morogoro kwa ajili ya maandalizi ya mechi yao dhidi ya Singida Fountain Gate utakaopigwa Agosti 31, mwaka huu.

“Kila kitu kimekwenda vizuri wachezaji wetu wapya tuliowasajili tumeshawaingiza kwenye mfumo na tunajipanga kwa mechi ijayo ya ligi kuhakikisha tunafanya vizuri na kupata matokeo mazuri baada ya kupoteza mechi ya kwanza dhidi ya Azam FC,” amesema Meneja huyo.

Naye Kocha Mkuu wa kikosi cha timu hiyo, Goran Kopunovic, amesema kabla ya kwenda kuweka kambi Morogoro alifanya kikao na viongozi wake na kumhakikishia hakutakuwa na changamoto yoyote ya kukosa wachezaji katika mechi ijayo.

Pia alizungumzia suala lake la kimkataba na kuahidiwa kufanyia kazi kwa kukamilishiwa kile ambacho walikubaliana katika mkataba wao walioingia.

“Nimezungumza na viongozi wangu kuhusu makubaliano yetu, lakini mustakabali wa timu kwa wachezaji ambao tumewasajili kuhakikisha kila kitu kinaenda vizuri niweze kuwatumia kwenye mechi yetu ijayo dhidi ya Singida Fountain Gate FC, limefanyiwa kazi na sasa tupo Morogoro kwa ajili ya maandalizi,” aesema Kocha Goran.

Chanzo: Dar24