Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tabora United yatakata nyumbani, waichapa Dodoma Jiji

Tabora Vs Dodom Tabora United yatakata nyumbani, waichapa Dodoma Jiji

Fri, 6 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Tabora United imeendelea kutamba kwenye Uwanja wake wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora baada ya leo kuibuka na ushindi wa mabao 2-1, dhidi ya Dodoma Jiji, katika mchezo mkali na wa kusisimua wa Ligi Kuu Bara.

Dodoma ilikuwa ya kwanza kupata bao la utangulizi kupitia kwa mshambuliaji, Yassin Mgaza dakika ya pili tu ya mchezo kisha Tabora kusawazisha kwa mkwaju wa penalti dakika ya 50, lililofungwa na nyota, Erick Okutu.

Wakati mchezo huo ukienda ukingoni, mshambuliaji Abbas Athuman aliyejiunga na timu hiyo msimu huu akitokea klabu ya Taifa Jang'ombe ya visiwani Zanzibar aliiandikia Tabora United bao la pili na la ushindi dakika ya 90.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: