Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tabora United yagomea likizo

Tabora United Www Tabora United yagomea likizo

Wed, 13 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Wakati Ligi Kuu ikisimama kwa muda kupisha kalenda ya kimataifa, Tabora United imesema haitarajii kupumzika badala yake kutumia muda huo kusahihisha makosa ili kukwepa kushuka daraja.

Timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu kwa mara ya kwanza, haijawa na matokeo mazuri, kwani majuzi tu ilishuhudiwa ikinyukwa mabao 4-2 na KMC na kuwa nafasi ya 13 kwa pointi 21 baada ya michezo 20.

Kwa sasa Ligi Kuu itasimama kwa takribani mwezi mmoja kupisha kalenda ya kimataifa ambapo Tabora United itarudi uwanjani Aprili 14 kuwakaribisha JKT Tanzania.

Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Henry Mkanwa alisema mapumziko hayo wanapaswa kuyatumia vyema kurekebisha makosa yao kiufundi ili wanaporudi uwanjani wafanye vizuri.

Alisema hawatarajii kwenda mapumziko badala yake wanaenda kuanza na safu ya ushambuliaji ambayo haijawapa kile walichotarajia, sambamba na beki iliyoonesha kuruhusu mabao.

“Tunaenda mapumziko kwa raha gani, hiki ni kipindi muhimu kwetu kutathimini na kurekebisha tulipokosea, eneo kama straika na beki tunapaswa kuyaangalia kwa jicho la tatu,” alisema Mkanwa.

Kocha huyo aliongeza kuwa kuhusu ratiba ya timu hiyo ikiwamo mechi za kirafiki wanaenda kukaa na uongozi kuweka mipango sawa kuhakikisha wanafanya vizuri na kujinusuru kushuka daraja.

“Mipango mingine ni lazima kukutana na uongozi kuweka mikakati, suala la kushuka daraja ni mapema sana kulizungumza kwa sababu mechi bado zipo na lolote linaweza kutokea,” alisema kocha huyo.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: