Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tabora United yafuata beki Mapinduzi Cup

Tabora United Al Hassan Mwinyi Tabora United yafuata beki Mapinduzi Cup

Mon, 8 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tabora United imethibitisha kwamba imetuma mtu wao wa kusaka vipaji kwenye mashindano ya Kombe la Mapinduzi kusaka beki wa kushoto.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Tabora United Thabit Kandoro amesema wamemtuma mtu maalum kisiwani huko kusaka beki mzawa wa kushoto kwa ajili ya kusajiliwa dirisha hili dogo la usajili.

Kandoro amethibitisha kuwa mastaa wao wa kigeni wapya watakaowasajili tayari wameshaanza kuwasili wakisubiri kuanza kwa mazoezi ya kikosi hicho.

"Tunaendelea na usajili wapo ambao usajili wao tumeshaukamilisha na wengine bado, hivi ninavyokwambia Kuna mtu wetu yupo Zanzibar tunamtafuta beki wa kushoto mzuri,"amesema Kandoro.

"Kocha anahitaji beki mzuri wa kushoto wapo ambao tumeshaanza kuwaona Sasa tumeona tumtume mtu huko kuona ni yupi tutamalizana naye aje kutuongezea kitu.

"Tunataka kukamilika sawasawa mapema tunafahamu kwamba ligi itakaporejea ushindani utakuwa mkubwa zaidi kwa hiyo ni lala salama kila timu itapigania roho yake."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live