Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tabora United yaendeleza ubabe Ali Hassan Mwinyi

Tabora Vs Dom Tabora United yaendeleza ubabe Ali Hassan Mwinyi

Fri, 6 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Tabora United imeendelea kutamba kwenye Uwanja wake wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora baada ya leo kuibuka na ushindi wa mabao 2-1, dhidi ya Dodoma Jiji, katika mchezo mkali na wa kusisimua wa Ligi Kuu Bara.

Dodoma ilikuwa ya kwanza kupata bao la utangulizi kupitia kwa mshambuliaji, Yassin Mgaza dakika ya pili tu ya mchezo kisha Tabora kusawazisha kwa mkwaju wa penalti dakika ya 50, lililofungwa na nyota, Erick Okutu.

Wakati mchezo huo ukienda ukingoni, mshambuliaji Abbas Athuman aliyejiunga na timu hiyo msimu huu akitokea klabu ya Taifa Jang'ombe ya visiwani Zanzibar aliiandikia Tabora United bao la pili na la ushindi dakika ya 90.

Bao la Yassin Mgaza ni la kwanza kwa nyota huyo akiwa na kikosi hicho tangu alipojiunga nayo akitokea KMKM ambayo alikuwa na msimu mzuri baada ya kumaliza mfungaji bora wa Ligi ya Zanzibar baada ya kufunga mabao 19.

Kwa upande wa mshambuliaji Eric Okutu hilo linakuwa bao lake la pili msimu huu tangu ajiunge na kikosi hicho akitokea klabu ya Heats of Lions ya nchini Ghana baada ya kufunga kwenye mchezo na Tanzania Prisons Septemba 15.

Katika mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora ilishinda mabao 3-1 ambapo mbali na raia huyo wa Ghana kufunga ila mengine yaliwekwa nyavuni na Mganda, Ben Nakibinge aliyefunga mawili peke yake.

Ushindi huu ni wa pili kwa Tabora kwenye uwanja huo msimu huu baada ya kuifunga Prisons huku ukiwa ni wa tano ambapo mbali na ushindi huo ila ilipoteza mmoja tu dhidi ya Azam kwa mabao 4-0 na kutoka sare miwili.

Kwa upande wa Dodoma Jiji hiki kinakuwa ni kipigo cha pili msimu huu baada ya kupoteza na Simba kwa mabao 2-0 dhidi ya Agosti 20 kwenye Uwanja wa Uhuru.

Katika michezo mitano ambayo pia Dodoma imecheza imeshinda mmoja tu wa mabao 2-1 dhidi ya Coastal Union Agosti 15, kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma huku ikichezea vichapo viwili na kutoka sare miwili.

Kwa matokeo haya, Tabora United inafikisha pointi nane ikiwa nafasi ya tano katika msimamo wa Ligi Kuu Bara huku kwa upande wa Dodoma Jiji inashika nafasi ya 10 na pointi tano baada ya zote kucheza michezo mitano.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live