Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tabora United yachimba mkwara Ligi Kuu Bara

Tabora United Mikwara.png Tabora United yachimba mkwara Ligi Kuu Bara

Thu, 30 Nov 2023 Chanzo: Dar24

Benchi la Ufundi la Tabora United, limefunguka kwamba, mashabiki wa timu hiyo hawapaswi kuwakatia tamaa kwani wameahidi kutembeza dozi kwa mechi zilizobaki wakianza na Mtibwa Sugar.

Kesho ljumaa (Desemba Mosi), Tabora United itakuwa mwenyeji wa Mtibwa Sugar katika muendelezo wa Ligi Kuu Bara, mechi ikichezwa Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora.

Ofisa Habari wa Tabora United, Pendo Lema, amesema nafasi waliyopo haiendani na hadhi yao, wataendelea kusahihisha makosa yao kwa mechi zilizosalia ili kuondoka na alama tatu kila mechi.

“Tuna wachezaji wazuri ambao kuwafunga basi ufanye kazi ya ziada ndiyo maana mara nyingi matokeo yetu yanakuwa sare kwa sababu kama tukishindwa kumfunga mpinzani basi na yeye atapata tabu kutufunga.

“Katika mechi zote ambazo tumeshacheza mpaka sasa, mechi ambayo tulifungwa mabao zaidi ya matatu ni ile mechi ya kwanza tu ambapo ilitokea dharura tukacheza pungufu, vinginevyo makosa hayo hayajajirudia hiyo inaonesha dhahiri kuwa wachezaji wetu wana kitu na kitu hicho wanaenda kukionesha mechi zilizóobaki,” amesema.

Chanzo: Dar24
Related Articles: