Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tabora United vs Yanga sasa kupigwa Dodoma

Yanga Hanang Tabora United vs Yanga sasa kupigwa Dodoma

Wed, 20 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), imefanya mabadiliko ya uwanja wa mchezo wa Ligi Kuu ya NBC kati ya Tabora United dhidi ya Yanga SC

Mchezo huo namba 110, ambao timu Yanga SC itakuwa ugenini, sasa utachezwa Desemba 23, 2023, saa 1:00 Usiku kwenye Uwanja wa Jamhuri uliopo Dodoma.

Awali mchezo huo ulipangwa kuchezwa Desemba 22, 2023, saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi uliopo mkoani Tabora.

Kwa mujibu wa TPLB, sababu za mabadilko hayo ni Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi kufungiwa na Kamati ya Leseni za Klabu ya TFF.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live