Timu ya Biashara United imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Tabora United katika mchezo wa kwanza wa mchujo wa kuwania kucheza Ligi Kuu msimu ujao leo Uwanja wa Karume, Musoma mkoani Mara.
Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee Herbert Lukindo kwa penaltı dakika ya 90’+9 na timu hizo zitarudiana Jumapili Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi mjini Tabora na mshindi wa jumla atacheza Ligi Kuu msimu ujao.
Biashara United imetoka Championship ambako iliitoa Mbeya Kwanza kwa kuifunga 2-0 nyumbani na ugenini, wakati Tabora United imeporomoka Ligi Kuu ya kufungwa kwa jumla ya mabao 4-0 na JKT Tanzania, 4-0 Tabora na 0-0 Mbweni.