Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tabora United ipo katika mtego kubaki Ligi Kuu Bara

Tabora United Milioni 50 Tabora United ipo katika mtego kubaki Ligi Kuu Bara

Thu, 6 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kwenye soka lolote linaweza kutokea hivyo hata Tabora United inaweza kufanya maajabu ya kupata ushindi mnono kwenye mechi ya marudiano ya mchujo dhidi ya JKT Tanzania, ugenini hiyo keshokutwa na kujihakikishia kubaki Ligi Kuu.

Lakini kiuhalisia, Tabora United ina kibarua kigumu kwani inatakiwa kupata ushindi wa kuanzia angalau mabao matano katika mechi hiyo itakayochezwa kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Dar es Salaam, Jumamosi hii ili ibaki.

Kama ikishindwa kutoboa mbele ya JKT Tanzania, maana yake itakutana na ‘Wanajeshi wa Mpakani’, Biashara ya Mara ambayo inapambana kucheza Ligi Kuu baada ya kupita katika mchujo wa Ligi ya Champioship.

Hii mechi dhidi ya Biashara United sio nyepesi kwa Tabora United na inatakiwa ifanye kazi kubwa sana vinginevyo inaweza kujikuta ikishuka rasmi daraja baada ya kucheza msimu mmoja.

Kwanza itakutana na Biashara United ambayo wachezaji wake wamepata nafasi ya kutosha ya kupumzika kwani tangu ilipofanya vizuri dhidi ya Mbeya Kwanza mwezi uliopita, haijacheza tena mechi ngumu ya kiushindani.

Ni tofauti na Tabora United ambayo yenyewe itakuwa imetoka kucheza mechi mbili ngumu dhidi ya JKT Tanzania na baada ya hapo inapaswa kusafiri hadi Mara kucheza na Biashara United.

Kingine ni ubora wa kikosi ambacho Biashara United inacho ambacho kina wachezaji wengi wenye uzoefu wa kucheza mechi ngumu kwa vile kinaundwa na wachezaji wengi waliowahi kucheza Ligi Kuu misimu michache iliyopita.

Mfano wa wachezaji wa Biashara United ambao waliwahi kucheza Ligi Kuu ni Boban Zirintusa, Mpapi Nassibu, Ramadhan Kipalamoto, Herbert Lukindo, Babilus Chitembe, Rehani Kibingu, Cyprian Kipenye na Robert Mapigano. Kuna shughuli pevu hapo, Tabora United isiichukulie poa Biashara United.

Chanzo: Mwanaspoti