Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Taarifa ya Simba kuhusu majeruhi ya Kapombe na Kibu Denis

Kapombe Kibu 08295 Taarifa rasmi kuhusu majeruhi ya Kapombe na Kibu Denis

Mon, 3 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Simba imebainisha kuwa wachezaji Shomari Kapombe na Kibu Denis ambao walipata majeraha kwenye mchezo wa kuhitimisha hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa dhidi ya Raja Casablanca, watafanyiwa vipimo kubaini ukubwa wa majeraha yao leo.

Kapombe na Kibu walishindwa kumaliza dakika zote tisini katika mchezo uliopigwa huko Morocco usiku wa kuamkia Jumamosi na Simba kupoteza kwa mabao 3-1.

Hata hivyo Daktari wa Simba Edwin Kagalo amewatoa hofu Wanamsimbazi kuwa uchunguzi wa awali wa majeraha ya Kapombe hayakuonekana kuwa makubwa hivyo beki huyo mahiri wa upande wa kulia anaweza kupewa mapumziko ya siku chache.

Nyota mwingine ambaye atafanyiwa vipimo ni winga Peter Banda aliyepata majeraha wakati akiwa kwenye majukumu ya timu ya Taifa.

Msimu huu haukuwa mzuri kwa Banda kwani majeraha yamekuwa changamoto kubwa kwake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live