Taarifa ya Bodi ya Ligi ikielezea Klabu ya Yanga SC kutozwa faini ya milioni kadhaa na Mwamuzi Florentina Zabron (Dodoma) kuondolewa kwenye ratiba ya waamuzi kwa mizunguko 6 na adhabu nyingine kibao.
Prisons vs Simba
Mwamuzi msaidizi namba mbili wa mchezo uliowakutanisha Prisons FC dhidi ya Simba SC, Nestory Livangala (Iringa) ameondolewa kwenye ratiba ya waamuzi kwa mizunguko mitano (5) kwa kosa la kushindwa kutafsiri vema sheria za mpira wa miguu katika mchezo uliotajwa hapo juu.
Katika mchezo huo Simba SC iliibuka na Ushindi wa magoli (1-3) dhidi ya Tanzania Prisons katika Dimba la Sokoine Mbeya
Singida vs Simba
Kamati ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imemwondoa Mwamuzi Msaidizi namba mbili wa mchezo wa Singida Fountain Gate dhidi ya Simba SC, Abdallah Bakenga kwenye ratiba ya waamuzi kwa mizunguko mitano, kwa kosa la kushindwa kutafsiri vema sheria za mpira wa miguu katika mchezo tajwa.
Ihefu vs Yanga
Klabu ya Yanga imetozwa faini ya shilingi milioni mbili kwa makosa (2)
◉ Tsh Million 1 kwa kosa la naashabiki wake kurusha chupa za maji uwanjani
◉ Tsh Million 1 kwa kosa la maofisa wa klabu ya Yanga wa benchi la ufundi kuonekana wakipinga maamuzi na kumzonga mwamuzi wa akiba.
◉ Kocha wa Ihefu, Zuberi Katwila amepigwa faini ya Tsh million 1 kwa kosa la kuwaambia watu wa huduma ya kwanza kutembea polepole wanapowatoa kwenye pitch wachezaji wa Ihefu ili kupoteza muda.
Pia, afisa habari wa Klabu ya Yanga, Ali Kamwe amepigwa faini ya Tsh Million 1 kwa kosa la kumshutumu mwamuzi, Tatu Malogo kwenye mtandao wa kijamii baada ya mechi ya Singida dhidi ya Simba SC.
Ally Kamwe alipost picha ya Tatu Malogo kisha akaweka wimbo wa 'MAOKOTO'.
Dodoma Jiji vs Azam FC
Klabu ya Azam FC imepewa onyo baada ya kuchelewa kuwasili uwanjani kwa dakika (8).