Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Taarifa kuhusu Azam FC kumtaka Kocha Moallin

Moallin Azam DC Taarifa kuhusu Azam FC kumtaka Kocha Moallin

Thu, 2 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kuibuka tetesi zinazoihusisha klabu ya Azam FC kuwa kwenye mpango wa kutaka kumrudisha kocha wao wa zamani Abdi Hamid Moallin kufuatia kufanya vizuri akiwa na KMC, Mtendaji Mkuu wa KMC Daniel Mwakasungula hakuna taarifa yoyote waliyopokea kutoka kwa kocha wao juu ya tetesi zinazoendelea.

“Sisi pia tunasikia na kuona kama ambavyo nyie mnasikia na kuona kupitia mitandao, mwalimu Moallin bado ana mkataba na KMC FC kwa hiyo kinachoendelea ni kwa sababu ameonesha uwezo mkubwa kwa hiyo hizo taarifa lazima ziwepo.”

“Hadi sasa kilakitu bado ni tetesi na mwalimu hajasema chochote, tunachojua sisi mwalimu anaendelea na majukumu yake kwa ajili ya maandalizi ya mechi zinazokuja za Ligi Kuu ya NBC.”

“Kama itatokea atatupa taarifa rasmi ya ofa aliyopata kutoka klabu nyingine hilo ni jambo jingine, lakini huwezi kumzuia mtu anapotaka kuondoka kwa sababu zake binafsi inabidi uheshimu.”

“Kwa ninavyomfahamu Moallin ni kocha mwenye weledi, msikivu na tayari alishakubali na kuendana na mazingira ya KMC FC, anafurahia maisha ya Kinondoni. Mwisho wa siku akiamua kuondoka tutaheshimu uamuzi wake.”

Inaelezwa kuwa, Azam FC ipo katika mpango wa kumrudisha Moallin Chamazi na tayari imefanya majaribio kadhaa lakini kocha huyo amepiga chini na ofa ya mwisho iliyotumwa na Azam kwa Moallin ni kiasi cha Tsh. 250 ili kumng’oa KMC lakini kocha huyo anaeamini katika vijana bado hajaijibu!

Je, Moallin ataendelea kuitolea nje Azam FC au nguvu ya pesa itamrudisha Chamazi?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live