Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TUTAENDA KUUTETEA UBINGWA WETU TENA

Capture 305?fit=832%2C541 TUTAENDA KUUTETEA UBINGWA WETU TENA

Mon, 20 Jul 2020 Chanzo: zanzibar24.co.tz

Katibu wa chama cha Riadha Zanzibar Muhidin Yassin Masuzu amesema kuwa suala la kuruhusiwa kwa shughuli za michezo Nchini wamelifurahia sana kwavile limekuja muda muafaka.

”Sisi Chama cha Riadha Zanzibar tumepokea kwa furaha kubwa na tunaipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuamua kutufungulia michezo kuendelea hasa mchezo wa riadha”

Yassin amesema ”Suala la kufunguliwa kwa michezo limekuja muda muafaka kwavile hivi karibuni tunatarajia kuingia katika mashindano ya Mikoa yanatarajiwa kuanza Mwanzoni mwa Mwezi wa Tisa, na katika michuano hiyo tunatarajia kurudi na ushindi kwa maranyengine tena”.

Muhidin ameeleza hatua watakayoanza nayo wao kama chama cha riadha kwa wale wakimbiaji waliomo ndani ya taasisi pamoja na vilabu “Tutaanza kwa kuvijuulisha vilabu vyote vya mchezo wa riadha na taasisi zote zenye wachezaji wa riadha ili wawaruhusu wachezaji kufanya mazoezi na kuwapa muda wa kutosha”

Katibu huyo pia ametoa ushauri wake kwa wanamichezo katika kufuata miongozo ya kiafya “Wachezaji wa riadha watakaporudi katika mazoezi ya pamoja waendelee kuchukua tahadhari ya virusi vya Corona kwani maradhi ya corona bado yapo”.amesema Katibu huyo wa chama cha riadha

Chanzo: zanzibar24.co.tz