Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TRA: Mtibwa Sugar tutaishi nao tu

TRA MTIMBWA TRA: Mtibwa Sugar tutaishi nao tu

Wed, 30 Nov 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya kupangwa na Mtibwa Sugar katika mchezo wa kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC) uongozi wa timu ya soka ya TRA FC 'La Familia' kutoka mitaa ya Njoro Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro imeweka wazi kuwa wako tayari na wala hawana presha yeyote.

TRA FC inashiriki First League huku Mtibwa Sugar wenyewe wakiwa Ligi Kuu Tanzania Bara ambapo timu hiyo imetinga katika hatua hiyo baada ya kuichapa Eagle SC kutoka mkoani Manyara mabao 3-1,mchezo ambao ulipigwa Novemba 20 mwaka huu katika uwanja wa Majengo Complex Moshi.

Mchezo kati ya Mtibwa Sugar dhidi ya TRA FC itapigwa kati ya Disemba 9-11,ambapo mwenyekiti wa TRA FC,Ally Hemed amesema wamepokea taarifa za kupangwa na vigogo hao kwa mshituko mkubwa lakini hakuna namna wako tayari kupambana na wala hawaogopi.

Amesema haya ni mashindano ya mtohano timu ambayo imejiandaa vyema ndio itaweza kuibuka na ushindi lakini pia kusonga mbele hivyo wao kwa sasa wanajipanga kwenda kumfunga Mtibwa kwake na kusonga wala siyo kingine.

“Tunajua tunakwenda kucheza na bingwa wa mwaka 2018 lakini ukumbuke pia waliwahi kutolewa na timu ndogo Sahare All Stars hapo hapo kwao katika mashindano haya hivyo hata sisi tunaweza kumtoa pia vile vile kama tutafanya maandalizi vyema”amesema Hemed.

Ameongeza kuwa wana waheshimu Mtibwa kwa kuwa wako katika daraja la juu zaidi yao pia wana wachezaji bora wenye uzoefu na mashindano yote lakini nao wajipange wakitambua watakutana na upinzani na siyo mchekea.

Mwenyekiti huyo pia ametumia fursa hiyo kuzungumzia maandalizi ya mchezo wa kundi A ya First League kati ya timu hiyo dhidi ya African Lyon ambayo itapigwa Jumamosi hii kwenye uwanja wa Majengo Moshi ambapo amesema kikosi chao kiko katika ari na morali kubwa kuhakikisha wanabakisha alama Tatu nyumbani.

Amesema Ligi hiyo ngumu kila timu inapambana lakini kikubwa kwao ni kutimiza malengo yao ambayo ni kutinga hatua ya Nane bora kisha kupambania kupanda Championship huku akitamba kutokana na ubora wao anaamini watafanikisha ilo.

TRA FC katika msimamo wa kundi A ya First League inashika nafasi ya Tano sawa na mechi ilizocheza,wakiwa na pointi Saba.Timu hiyo imeshinda mechi Mbili sawa na iliyopoteza huku ikitoka sare Moja,ambapo pia imefunga magoli matano na kufungwa Saba.

Chanzo: Mwanaspoti