Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TPLB yasogeza mbele mchezo wa Simba dhidi ya Mbeya City

Uwanja Wa Mkapa 1140x640 TPLB yasogeza mbele mchezo wa Simba dhidi ya Mbeya City

Fri, 13 Jan 2023 Chanzo: Dar24

<

Bodi ya Ligi Tanzania Bara ‘TPLB’ imefanya mabadiliko ya Rabita ya Ligi Kuu Tanzania Bara, kwa kusogeza mbele tarehe ya mchezo namba 157, kati ya Simba SC dhidi ya Mbeya City.

Mchezo huo ulipangwa kupigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa Jumanne (Januari 17), na sasa utachezwa Jumatano (Januari 18) katika Uwanja huo.

Sababu kuu ya kusogezwa mbele kwa mchezo huo ni kuipa Simba SC nafasi ya kufanya safari yake ya kurejea nchini Ikitokea Falme za Kiarabu, ambako imeweka kambi ya maandalizi.

Katika hatau nyingine Singida Big Stars ambayo leo Ijumaa itacheza mchezo wa Fainali Kombe la Mapinduzi 2023 dhidi ya Mlandege Kiziwani Unguja ‘Zanzibar’, mchezo wake wa ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar haujafanyiwa mabadiliko.

Kwa mantiki hiyo timu hizo zitacheza mchezo namba 153 Jumanne (Januari 17) katika Uwanja wa Liti mjini Singida, saa kumi jioni.

Chanzo: Dar24