Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TP Mazembe yatupwa nje Ligi ya Mabingwa Afrika

Mazembe Out TP Mazembe imetolewa kwa mikwaju ya Penati 4-2

Sat, 15 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wababe wa Soka la Afrika, Timu ya TP Mazembe kutoka DR Congo imetupwa nje katika michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika.

Mazembe waliokuwa wakipambana kuwania kufuzu kwa hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Arika, wamelazimishwa sare ya bila kufungana na Vipers FC ya nchini Uganda na hivyo kutolewa kwa njia ya matuta (4-2).

Katika mchezo wa Mkondo wa kwanza timu hizo zilienda sare ya bila kufungana, na mchezo wa leo mpaka dakika 90 zinakamilika matokeo yalikuwa 0-0.

Katika changamoto ya mikwaju ya penati ndipo Vipers walipopata nafasi ya kuandika historia ya kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mara ya kwanza baada ya kuibuka wababbe kwa penati 4-2.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live