Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TP Mazembe wamponza mwamuzi, achezea kipigo (+Video)

Video Archive
Fri, 17 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwamuzi aliechezesha mchezo wa Ligi Kuu ya wanawake Congo kati ya DC Motema Pembe na TP Mazembe alilazimika kukimbia ili kuokoa uhai wake baada ya kushambuliwa na wachezaji wa DC Motema Pembe.

Mwamuzi huyo alikubwa na dhahama hiyo baada ya kukataa kuwazawadia Motema Pembe mkwaju wa Penati.

Wakati DC Motema Pembe wakilalamikia kunyimwa Penati, tayari walikuwa nyuma kwa magoli 5-1.

Wachezaji wa DC Motema Pembe malijaribu kumkimbiza mwamuzi aliejitahidi kukimbia lakini alijikuta mikononi mwa wachezaji hao na wakaanza kumshambulia katika maeneo mbalimbali ya mwili wake.

Katika baadhi ya Vipande vya Video, wachezaji wa Timu ya Motema Pembe wanaonekana wakimpiga mwamuzi huku mwanaume mmoja anaesadikiwa kutoka katika benchi lao la ufundi akishiriki pia.

Wakati tukio hilo likitokea wachezaji wa Timu ya wanawake ya TP Mazembe walibaki Uwanjani wakishuhudia tukio hilo.

Chama cha Soka nchini Congo tayari kimewafungia baadhi ya Wachezaji na wameanza uchunguzi kuhusiana na tukio hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live