Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TP Mazembe wamfuata Kelvin John

63834 Pic+mazembe

Sat, 22 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

VIGOGO wa Klabu tajiri ya TP Mazembe wako jijini Dar es Salaam tangu jana Alhamisi kwa ajili ya mambo makubwa mawili.

Viongozi hao, Mario Kawel na Patrick Kasangala wametumwa na klabu hiyo kuhakikisha wanawashawishi wasimamizi wa mchezaji kinda, Kelvin John 'Mbappe' pamoja na wazazi wake ili kuichezea timu yao.

Tayari wameanza kuzungumza na wasimamizi hao na sehemu ya ofa ni kumsomesha kwa kipindi atakachokuwa kwa sababu Mbape bado hajafikisha miaka 18.

Kasangala amesema, bado wanaendelea na mazungumzo lakini wasimamizi wake kama wana uoga juu ya mchezaji huyo kwa sababu ya udogo wa umri wake.

"Tunaendelea na mazungumzo kwa ajili ya Mbappe tunawasikilizia wasimamizi wake. Lakini tangu tumeanza kuongea nao kama wana uoga kikubwa wanachozungumza ni umri wake lakini hiyo kwetu haina shida,"alisema Kasangala.

Amesema, wao wamewahakikishia walezi wake Mbappe ambaye amekuwa akifanya vizuri kwenye soka kwa sasa hasa alipokuwa na timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 'Serengeti Boys' kuwa atakuwa salama.

Pili, unaweza kusema kama wameingia anga za Simba na Yanga kwa sababu wanawasaka beki wa kushoto, Mohamed Hussein 'Tshabalala' na kiungo, Feisal Salum 'Fei Toto' ambao wote si wachezaji huru.

Mabosi hao wanafanya mpango wa kuzifikia klabu zao Yanga kwa ajili ya Fei Toto na Simba, Tshabalala.

Inadaiwa TP Mazembe wamejipanga kupeleka ofa kwa ajili ya wachezaji hao ambao wote kwa sasa wako nchini Misri na timu ya Taifa Stars katika fainali za AFCON zinazoanza kutimua vumbi leo Ijumaa.

Awali, TP Mazembe ilikuwa tayari kumsajili Ibrahim Ajibu anayemaliza mkataba wake Yanga kwa dau la dola 50,000 (zaidi ya Sh 120milioni) na mshahara wa dola 5000 (zaidi ya 12 milioni) kila mwezi  lakini klabu hiyo inayomilikiwa na mfanyabiasha mkubwa na mwanasiasa nchini Congo, Moise Katumbi, walishindwa kufanikisha.

"Timu inatafuta beki wa kishoto na kiungo na hao wachezaji ndio wanalengwa lakini kwa sababu wana mikataba na klabu zao lazima kumalizana na Simba na Yanga kwanza ndio watupe wachezaji,"alieleza Kasangala.

TP Mazembe tayari imemsajili straika Mtanzania, Eliud Ambokile kutoka Mbeya City.

Chanzo: mwananchi.co.tz