Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TP Mazembe, msimu mbaya kwa Kunguru alielala

TP Mazembe Squad Salary Kikosi cha TP Mazembe

Tue, 21 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hawa TP Mazembe ukifika geti kuu la kuingia uwanjani kwao kuna Kunguru wa kuchongwa amekanyaga mpira, Ndani ya kuta za uwanja kuna michoro ya Mamba anatafuta mpira.

Njia ya kutoka kwenye vyumba vya kubadilishia nguo kuna michoro ya mastaa wao waliowahi kufanya makubwa na TP, Akiwemo Mbwana Samata pia.

Ukiingia Uwanjani wakati vikosi vinaelekea kwenye Pitch kabla ya mchezo kuanza mashabiki wanasimama na kunyoosha mkono mmoja juu maana yake Kunguru anapaa.

Baada ya picha ya kikosi, Wanapita kwa kukimbia katikati ya mstari unaogawa uwanja kwa kufuatana kisha wanatawanyika, wakiashiria Kunguru wanaachana hewani.

Hii yote ni mikwara tu, Wanatengeneza hofu kwa mgeni, miaka ya nyuma ilikua ngumu kushinda Lubumbashi lakini kwa sasa heshima hiyo imepotea. Mazembe ina anguko kubwa.

Mmiliki wa timu Moise Katumbi kuelekea kampeni ya CAF Msimu huu aliwasisitiza Mashabiki kwenda uwanjani kwa wingi baada ya kuonekana kususia baada ya kupoteza kwa Vipers SC ya Uganda.

Mashabiki wakajitokeza kwa wingi kwamba wamekubali kua hawapo Ligi ya mabingwa wapo Shirikisho, Mpango wa Mazembe ukawa kubeba taji hili msimu huu.

Cha ajabu wameshafungwa mechi 4, mpaka Sasa na Yanga anaenda kumalizana nae kwake, Haiaminiki kama Inawezekana lakini ndio uhalisia tunaouona.

Huu ni msimu mbaya kwa Kunguru alielala, hatujui Ligi Kuu watamalizaje safari ya msimu huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live