Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TFF yazipongeza Yanga na Coastal Union

Tff Yanga.jpeg TFF yazipongeza Yanga na Coastal Union

Sun, 3 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imezipongeza timu za Yanga na Coastal Union ya Tanga kwa mchezo mzuri wa Fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) uliochezwa jana kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha.

Katika taarifa iliyotolewa na TFF imezipongeza timu hizo kwa kuonyesha kiwango kizuri cha ushindani hadi kumpata bingwa wa ASFC kwa msimu wa 2021/22.

Taarifa hiyo iliendelea kwa kuzipongeza timu zote mbili, Yanga ambao ndio Mabingwa na Coastal Union waliochukua nafasi ya pili.

Aidha TFF imewashukuru mashabiki wote wa Mpira wa Miguu kwa kujitokeza kwa wingi viwanjani msimu mzima na kuziunga mkono timu zao.

TFF inaamini kwamba mashabiki ni sehemu muhimu katika maendeleo ya Mpira wa Miguu hivyo inawashukuru kwa wakati wao wa kuunga mkono mashindano mbalimbali kwa kujitokeza kwa wingi uwanjani msimu mzima.

Katika mchezo huo Yanga iliibuka kidedea kwa mikwaju ya penalti 4-1, kufuati mchezo huo kumalizika kwa timu hizo kufungana mabao 3-3 ndani ya dakika 120.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live