Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TFF yavikumbusha vilabu kulipa leseni za wachezaji

Mechi Ya Mtibwa Vs Simba Kuhamishiwa Jamhuri Morogoro TFF yavikumbusha vilabu kulipa leseni za wachezaji

Thu, 14 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limezikumbusha Klabu zote za Ligi Kuu ya NBC, NBC Championship, First League na Ligi Kuu ya Wanawake ya Serengeti Lite kulipia na kuchukua leseni za wachezaji waliowasajili kwa msimu wa 2023/2024.

Kupitia taarifa yake kwa umma, TFF imesisitiza kuwa mchezaji ambaye hatakuwa na Leseni zilizochapishwa (printed) hataruhusiwa na kubainisha kuwa leseni za nakala laini (soft copy) hazitatumika.

Aidha TFF imezikumbusha klabu kulipa ada ya ushiriki na ada ya wachezaji wa kigeni na na kuzitaka klabu kufika Makao Makuu ya TFF, Karume, Ilala na nakala ya malipo ya ada ya ushiriki, malipo ya leseni za wachezaji na ada ya wachezaji wa kigeni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: