Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TFF yavikumbusha vilabu kuelekea kufungwa kwa Dirisha la Usajili

TIEFU EFUU TFF Ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Tue, 31 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limeendelea kuvikumbusha vilabu vinavyoshiriki ligi kuu, Championship, First League na Ligi kuu ya Wanawake (Serengeti Lite) kuhakikisha kuwa wanakamilisha usajili mapema na kwa wakati.

Taarifa ya TFF, imekuja wakati ambao kwa takribani miaka mitatu kumekua na malalamiko kutoka kwa baadhi ya vilabu wakilalamikia muda na kuna nyakati huongezwa muda wa ziada kwa dharura lakini safari hii hakutakua na muda wa ziada.

Dirisha la Usajili nchini litafungwa leo Agosti 31,2021, Majira ya saa sita usiku kwa saa za Afrika ya Mashariki.

Sehemu ya taarifa iliyotolewa na TFF

Chanzo: www.tanzaniaweb.live