Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TFF yataka Uwanja wa Majengo, Moshi kumalizika

Wallace Karia Bila Vijana Rais wa TFF, Wallace Karia

Sat, 29 Apr 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeitaka Halmashauri ya Manispaa ya Moshi kumalizia kujenga Uwanja wa Majengo ili ikiwezekana waweze kuipeleka nusu fainali au fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC).

Akizungumza Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia wakati alipozuru kujua maendeleo ya fainali za Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL Finals 2023) zinazoendelea kwenye uwanja wa Majengo, Moshi hatua ya nane bora.

Karia aliiahidi Manispaa ya Moshi endapo watafanya marekebisho ya uwanja wa Majengo Kama walivyokubaliana awali kuna uwezekano Mashindano ya FA katika ngazi ya Nusu fainali au fainali kufanyika hapo.

"Niliwaahidi kama watakamilisha hayo basi kama sio Fainali ya FA au nusu fainali inaweza ikachezwa kwenye Uwanja huo" alisema Karia.

"Kuna maeneo mengine ambayo hayajakuwa tayari kwa mfano vyumba vya kubadilishia nguo lakini pia kuna huduma za vyoo,majukwaa na uzio katika uwanja mzima" alisema na kuongeza

Aidha Karia aliongeza kuwa madhumuni ya kuitaka Manispaa ya Moshi iharakishe mpango kazi huo ni kuwa na Viwanja vingi nchini ili kuinua soka katika mazingira yaliyobora na rafiki kwa wanamichezo.

"Nausihi uongozi wa Kilimanjaro kwa maana ya serikali,federation wahakikishe huu Uwanja wanakamilisha ili angalau tuwe na Kiwanja kingine kwenye viwanja vyetu Tanzania ambavyo tunaweza kuvitumia kwa mashindano mbalimbali ya kitaifa na hata ya kimataifa" alisema Karia.

Ligi ya Mabingwa wa mikoa (RCL 2023) hatua ya nane bora imezijumuisha timu za Tanesco Fc (Kilimanjaro),Kiluvya Fc (Dar es salaam), Annuary Fc (Shinyanga), Tanzania Navy (Dar es salaam),Ilula Tigers (Iringa),Malimao Fc (Katavi),Mapinduzi Fc (Mwanza), na Nyumbu Fc ya Mkoani Pwani.

Chanzo: Mwanaspoti