Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania limevisimamisha viwanja vitano kutumika katika michezo ya Ligi Kuu ya NBC kwa msimu ujao kutokan na kutokidhi vigezo.
Viwanja hivyo vitano vilivyosimamishwa ni pamoja na Mkwakwani (Tanga), Nyankumbu Girls (Geita), Ushirika (Moshi), Mabatini (Pwani) na Jamhuri (Dodoma).
Wakati viwanja hivyo vikifungiwa, viwanja vya Majaliwa kilichopo Ruangwa, Sokoine (Mbeya) na Kaitaba (Bukoba) vimeagizwa kukamilisha marekebisho.
Jumla ya Viwanja tisa vimeruhusiwa kutumika kwenye michezo ya Ligi Kuu ya NBC msimu ujao ambapo viwanja hivyo ni pamoja na Benjamin Mkapa (DSM), Kirumba (Mwanza), Chamazi (DSM), Highland Estate (Mbarali, Mbeya), Karatu (Arusha), Liti (Singida), Manungu (Turiani, Morogoro), Amri Abeid (Arusha) na Uhuru (DSM)