Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TFF yampunguzia adhabu Haji Manara

Manara Karia Hm Karia na Manara

Thu, 15 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kamati ya rufaa ya Shirikisho la Mpira wa Miguu TFF leo imetangaza kumpunguzia adhabu Msemaji wa Yanga Haji Manara kutoka milioni 20 ya faini aliyotakiwa kuilipa hadi milioni 10 huku hukumu ya kufungiwa kujihusisha na soka kwa miaka miwili ikibaki palepale.

Mwenyekiti wa kamati ya rufaa ya Maadili ya TFF Richard Mbaruku amesema hii ni baada ya kupitia rufaa ya Haji Manara ambayo hata hivyo wameona haina mashiko lakini wakatumia busara ya kumpunguzia faini hiyo.

July 21 2022 Haji Manara alitangazwa kufungiwa miaka miwili kujihusisha na soka pamoja na faini ya milioni 20 baada ya kukutwa na hatia ya kumkosea nidhamu Rais wa TFF Wallace Karia wakati wa mechi ya fainali ya ASFC kati ya Yanga na Coastal Union Arusha Julai 2, 2022.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live