Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TFF yamfungia maisha Rais wa Klabu

Faruk Koca D TFF yamfungia maisha Rais wa Klabu

Fri, 15 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa Rais wa Klabu ya Soka ya MKE Ankaragucu ya nchini Uturuki, Faruk Koca amefungiwa maisha kujihusisha na masuala ya soka baada ya kumpiga ngumi mwamuzi mwishoni mwa mechi dhidi ya Caykur Rizespor ambapo mechi iliisha kwa sare ya 1-1.

Faruk Koca alikamatwa baada ya kumpiga muamuzi Halil Umut Meler mwishoni mwa mechi ya Super Lig Jumatatu usiku.

Shirikisho la Soka la Uturuki (TFF) limefikia uamuzi huo wa kumfungia Faruk Koca huku klabu ya MKE Ankaragucu ikipewa adhabu ya kulipa faini ya lira milioni mbili (£54,000) sawa na zaidi ya milioni 149 za kitanzania.

Timu hiyo pia imetakiwa kucheza michezo mitano ya nyumbani bila mashabiki kutokana na machafuko hayo yaliyohusisha mashabiki na viongozi wa klabu.

Mechi katika ligi zote za soka nchini Uturuki zilisitishwa kwa muda usiojulikana baada ya Koca kukimbia uwanjani na kugonga wavuni baada ya timu yake kukubali bao la kusawazisha dakika ya mwisho dhidi ya wapinzani wao Rizespor.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live