Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TFF yakunjua makucha Ligi Kuu ya Wanawake

TIEFU EFUU TFF TFF yakunjua makucha Ligi Kuu ya Wanawake

Sat, 15 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Timu ya Ligi Kuu ya Wanawake , Ceasiaa Queens imelimwa faini ya Sh 2 milioni na baadhi ya maofisa na wachezaji wa timu hiyo kuadhibiwa kwa kosa la kufanya vurugu na kuvunja pambano la ligi hiyo iliyokuwa imeshinda kwa mabao 2-1 dhidi ya Alliance Girls.

Pambano hilo lililopigwa Juni 11, kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Ceasiaa ilishinda mabao 2-1, lakini ilivunja pambano dakika ya 88 wakati mwamuzi Agneta Issack kutoka Kagera kuashiria penalti kwa wenyeji Alliance na maofisa wa timu wageni walimvamia na kumpuga mwamuzi huyo na pambano kuvunjika.

Leo Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetoa taarifa ya Kamati ya Soka la Wanawake kuinyang’anya ushindi Ceasiaa na kuizawadiwa Alliance pointi tatu na mabao matatu, huku ikiilima klabu hiyo Sh 2Milioni kwa mujibu wa kanuni ya 33 (1) na 33(6) za Kanuni za WPL.

Pia kamati hiyo, imemfungia kwa muda wa miezi sita na faini ya Sh500,000 kila mmoja, Meneja wa timu hiyo,Tedson Haule, meneja msaidizi, Jumanne Musuba, Kocha wa Makipa, Bashir Twalib na mchezaji, Khadija Mwita kwa kuhusika na vurugu za kumshambulia mwamuzi huyo.

Chanzo: Mwanaspoti