Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TFF yakubali kulipa mamilioni kampuni ya Romario Sports

TIEFU EFUU TFF TFF yakubali kulipa mamilioni kampuni ya Romario Sports

Tue, 20 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limefikia makubaliano nje ya mahakama katika shauri la madai lililokuwa limefunguliwa na kampuni ya Romario Sports 2010 Limited, kwa kuilipa kampuni hiyo deni pamoja na fidia.

Kulingana na hukumu ya makubaliano (consent judgement) iliyotolewa na Jaji Isaya Arufani wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, TFF itailipa kampuni hiyo jumla ya Sh1.69 bilioni kama deni pamoja na fidia mbalimbali.

Kiini cha mgogoro huo ni hatua ya TFF kutolipa deni la Sh843 milioni lililotokana na kampuni ya Romario Sports 2010 Limited, kuiuzia TFF vifaa mbalimbali vya michezo vyenye thamani ya Sh 893 milioni na hivyo kuingia katika mgogoro.

Baada ya TFF kushindwa kulipa deni hilo, kampuni hiyo iliwasiliana na TFF ili kujaribu kumaliza suala hilo kwa njia ya amani na wakakubaliana na TFF kuwa wangelipa fedha hizo kwa awamu 18 kuanzia Januari 31, 2023 hadi Juni 30,2024.

Hata hivyo, makubaliano hayo ya kumaliza deni hilo kwa njia ya amani hayakuzaa matunda na kusababisha kampuni hiyo kuamua kufungua shauri la madai namba 9792 la 2024 katika mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam.

Katika kesi hiyo, kampuni hiyo ilikuwa inaiomba mahakama itamke kuwa TFF imevunja makubaliano waliyoingia Februari 2,2023, walipe deni lote wanalodaiwa, kulipa fidia ya jumla ya Sh200 milioni na kulipa fidia ya hasara ya Sh300 milioni.

Pia mahakama iamuru TFF kulipa riba ambayo mahakama itaamuru kama fidia ya uharibifu na fidia ya jumla ambayo jumla yake ni Sh500 milioni na riba hiyo italipwa katika viwango vya kibiashara vinavyotozwa na mabenki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live