Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TFF yakanusha kumuombea Kibu uraia

Karia 1 Rais wa TFF, Wallace Karia

Tue, 5 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linakanusha taarifa inayosambazwa mtandaoni inayomuhusisha Rais wa TFF Wallace Karia na suala la uraia wa mchezaji Kibu Denis.

Taarifa hiyo inayosambazwa yenye nia ovu, inamnukuu Rais Karia akisema TFF imemuombea uraia Kibu kwa kuwa inamuhitaji na suala la utaifa wake ni jukumu la uhamiaji.

Taarifa hiyo inayosambaa sio ya kweli na kwamba Rais Wallace Karia hajatoa kauli hiyo kokote hivyo kuendelea kuisambaza ni kukiuka sheria za makosa ya mtandao. TFF ina utaratibu mzuri wa kutoa taarifa zake na kuzungumza na vyombo vya habari hivyo inawataka wote wanaosambaza taarifa hiyo ya upotoshaji kuacha mara moja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live