Mtendaji wa Bodi ya Ligi Kuu Almas Kasongo amesema Ratiba ya Ligi Kuu imepangwa kwa kuhakikisha wanapunguza idadi ya viporo
Kasongo amesema ratiba ya mechi za Kimataifa imepelekea kuonekana timu nyingine hazichezi muda mrefu
"Katika misimu miwili tumefanya kazi kubwa ya kuboresha ratiba ili kupunguza viporo.Tunafahamu huko nyuma malalamiko yalikuwa mengi kuhusu viporo"
"Zamani tulikuwa na timu moja au mbili zinazoshiriki mashindano ya CAF (Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho) lakini sasa tuna timu nne"
"Hivyo tunalazimika kusimamisha ratiba kwa timu zote kusubiri kukamilika kwa ratiba ya mechi za CAF. Utaona kwenye ratiba baadhi ya mechi hazijapangiwa tarehe kwa sababu tunasubiri kuthibithibisha ratiba ya mechi za CAF," alisema Kasongo.