Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TFF yafunguka adhabu ya Manara

Haji Manara Sd TFF yafunguka adhabu ya Manara

Tue, 23 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Saa chache baada ya Msemaji wa Yanga, Haji Manara kutangaza kurejea katika majukumu aliyokuwa anafanya awali, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limetoa baraka zote.

Manara jana, alitangaza kurejea kazini baada ya kumaliza adhabu ya kufungiwa kwa miaka miwili iliyotolewa na Kamati ya Maadili ya TFF. TFF kupitia Ofisa Habari, Clifford Ndimbo, amesema Manara yuko huru kuendelea na majukumu yake baada ya kukamilika kwa adhabu.

Ndimbo amesema, mbali na Manara kumaliza adhabu, pia amelipa kiasi cha Sh 10 Milioni ikiwa ni faini iliyoambatana na kifungo hicho.

"Manara yuko huru kweli, na hata huo mkutano alioufanya hajakosea kitu kwa kuwa hajafanya kosa lolote kikanuni, adhabu yake ulimalizika," amesema Ndimbo na kuongeza;

"Ukiacha kumalizika kwa adhabu yake pia TFF Ilishapokea malipo ya faini yake ya sh 10 Milioni, malipo hayo aliyafanya wikiendi iliyopita."

Manara alikumbana na adhabu hiyo kutokana kudaiwa kufanya makosa ya kimaadili alipokwaruzana na Rais wa TFF, Wallace Karia, katika Fainali ya Kombe la FA kati ya Yanga dhidi ya Coastal Union ya Tanga, uliochezwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: