Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TFF yafafanua Dkt. Ndumbaro kufungiwa

Ndumbaro Pic Data Dkt. Damas Ndumbaro.

Sat, 2 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa ufafanuzi kuhusiana na taarifa zinazoenea mitandaoni kuhusu kufungiwa kwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt.Damas Ndumbaro, na kubainisha kuwa, Waziri Dkt.Ndumbaro alifungiwa miaka saba na uongozi uliopita wa TFF lakini alikata rufani katika Kamati ya Rufani ya Nidhamu ya TFF kupinga adhabu hiyo.

Taarifa ya TFF imebainisha kuwa, Kamati ya Rufani ya Nidhamu ya TFF chini ya uongozi wa sasa ilisikiliza rufani hiyo mwaka 2017, ambapo Waziri Dkt.Ndumbaro alishinda, hivyo kuondolewa adhabu ya kufungiwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live