Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TFF wakana kuhusika na Wadukuzi wa Mitandaoni

Tff Waikana TFF wakana kuhusika na Wadukuzi wa Mitandaoni

Thu, 20 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa taarifa kuuarifu umma kuwa halihusiki na taarifa ya kundi la udukuzi mitandaoni la Anonymous kupinga Muswada wa Sheria ya Fedha wa Serikali ya Kenya.

Taarifa ya TFF ya leo Juni 20, 2024 imeeleza kuwa kundi hilo likitumia akaunti inayoonesha kuwa ni ya wenyeji wa Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) zitakazofanyika mwaka 2027 limechapisha katika ukurasa huo taarifa ya kupinga muswada huo.

“Tanzania, Kenya na Uganda ni wenyeji wenza wa fainali hizo za Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).” — imesema TFF

“Tunasisitiza kuwa TFF ikiwa ni mwanachama was Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) pamoja na CAF haijihusishi na masuala ya kisiasa kwa njia yoyote ile.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live