Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TFF mnasubiri dabi ipite?

Fei Toto Mudathri TFF mnasubiri dabi ipite?

Thu, 2 Nov 2023 Chanzo: Mwananchi

Kwa kawaida baada ya michezo ya ligi kuchezwa kuna kamati inaitwa ya saa 72 ambayo kazi yake kubwa ni kuja na mfululizo wa matukio ambayo kwa namna moja au nyingine yamevunja kanuni kwa Ligi za madaraja mbalimbali ikiwemo ligi Kuu.

Ni muda sasa tangu kuchezwa kwa mechi za ligi kuu raundi ya saba na ya nane lakini bado kamati hiyo ipo kimya na haijatoa maamuzi yeyote japokuwa yametokea na yanafahamika.

Kuanzia tukio la mashabiki wa Simba kumbutua shabiki wa Yanga lakini pia kuna kituko kilichotokea mechi ya Yanga na Azam FC iliochezwa tarehe 23 ya mwezi uliopita lakini kamati hiyo bado ipo kimya, kuhusu Feisal Salum na Mudathir Yahya kutegeana kuingia uwanjani.

Ukimya huo huenda wanaisubiri mechi ya Simba na Yanga ipite? Jibu linaweza kua ndio au hapana,ndio kama watatoa adhabu hizo baada ya mechi na hapana kama watakuja na sababu za kutuambia kwanini maamuzi yamechukua muda kufanyika.

Chanzo: Mwananchi