Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TFF kuwaburuza kortini mmliki wa Gwambina FC na Clouds FM

Gwambina Pic Msk TFF kuwaburuza kortini mmliki wa Gwambina FC na Clouds FM

Tue, 17 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limewaelekeza wanasheria wake kuchukua hatua dhidi ya Mmiliki wa Klabu ya Gwambina na kituo cha radio cha Clouds FM kwa madai ya kutoa taarifa za uongo juu ya shirikisho hilo.

Inadaiwa kuwa mmiliki wa Gwambina FC, Alexander Mnyeti amesema aliombwa shilingi milioni tano ya TFF ili aruhusiwe kutumia uwanja wake wa nyumbi ambao ulikuwa umefungiwa.

Aidha, timu ya Gwambina imejiondoa katika mashindano (league) championship ???? hii baada ya mmiliki wa klabu hiyo ambaye no mbunge wa Misungwu kuilalamikia TFF kuufungia uwanja wao wa nyumbani na kuwapangia mwingine (usafili watajwa).1

Hivi karibuni Gwambina liligomea Uwanja wa Nyamagana, Mwanza ikidai inaonewa kupelekwa michezo ya nyumbani katika uwanja huo.

Gwambina ilikumbana na rungu la faini ya Sh2 milioni pamoja na kupokwa alama 15 baada ya kutofika uwanjani katika mchezo dhidi ya African Sports na wiki hii haijatokea uwanjani kucheza na Mbuni.

Gwambina inaburuza mkia ikiwa na alama saba kabla ya hapo ilishakumbana na faini ya Sh1 milioni kwa kuchelewa kufika uwanjani licha ya kuwa nyumbani.

Hata hivyo, inaelezwa hadi sasa wachezaji wengi wameondoka kambini kutokana na sintofahamu hiyo pamoja na ukata unayoikumba Gwambina.

Katibu wa Gwambina, Daniel Kirai alisema wachezaji wamepewa ruhusa ya kutafuta timu na hilo lilikuwepo tangu awali waliwapa uhuru wachezaji wao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live