Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TFF itaje kikosi cha Stars hadharani - Ally Mayai

Taifa Stars Saudia Taifa Stars.

Tue, 17 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkurugenzi Mkuu wa Maendeleo ya Michezo nchini Ally Mayai Tembele amesema Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania 'TFF' lirudishe desturi ya kuwatangazia Watanzania kikosi cha Taifa Stars ili waweze kuwafahamu wachezaji wa kikosi hicho.

Mkurugenzi wa Michezo, Ally Mayai amesema Watanzania wamezoea kutangaziwa kikosi na sio njia ya sasa ambayo wameshtukia timu tayari ipo kambini kujiandaa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Sudan ambao usiku wa jana umemalizika kwa sare 1-1.

''Ninaaamini TFF italifanyia kazi suala hili ili warudshe ule utaratibu uliokuwepo mwanzo utakaowasaidia watanzania kuifahamu timu yao ili wapate muda wa kumchambua mchezaji mmojammoja,'' amesema Tembele

Katika hatua nyingine Tembele amekipongeza kikosi cha timu hiyo kwa kupata sare ya bao 1-1 dhidi ya Sudan kwenye mchezo wa kirafiki wa Kimataifa ambao umechezwa Jumapili ya jana Oktoba 15, 2023 nchini Saudi Arabia.

''Wachezaji walionyesha uwezo ambao kocha wao Mkuu tayari amepata na kuona kile alichokuwa anakihitaji.''amesema Tembele.

Ikumbukwe Stars ipo tayari na harakati za kuwania tiketi ya kushiriki Kombe la Dunia katika fainali zitakazofanyika 2026 katika nchi za Canada, Marekani na Mexico ambapo mechi zake za kuwania kufuzu zitaanza mwezi ujao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live