Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TFF imetangaza kumfungia Obrey Chirwa wa Yanga

1362 Sequence 01.Still036

Mon, 15 Jan 2018 Chanzo: millardayo.com

Baada ya wiki iliyopita kamati ya nidhamu ya shirikisho la soka Tanzania TFF kushindwa kufanya maamuzi ya kesi ya utovu wa nidhamu wa mchezaji wa kimataifa wa Zambia anayeichezea Yanga Obrey Chirwa kutokana na kushindwa kufika katika kesi hiyo.

Jumapili ya January 14 2018 kamati ya nidhamu ya TFF ilikaa na kumsikiliza Chirwa kabla ya kutoa adhabu, Chirwa alituhumiwa kwa utovu wa nidhamu aliyouonesha wakati wa mchezo wa Yanga dhidi ya Tanzania Prisons.



Baada ya kupewa nafasi ya kusikilizwa na kujitetea kamati ya nidhamu ya TFF ilitangaza kumfungia Chirwa mechi tatu, kaimu afisa habari wa TFF Cliford Ndimbo amethibitisha taarifa hizo “Chirwa alikiri kosa kwamba kweli ametenda kosa hilo, hivyo kamati imemfungia mechi tatu na faini ya Tsh 500,000”

Kutokana na adhabu hiyo Chirwa sasa ataukosa mchezo wa Yanga dhidi ya Mwadui January 17 2018, Yanga vs Njombe Mji January 21 2018 na mchezo wa Yanga vs Majimaji January 28 2018.



UTANI: Kwa nini Edo haizungumzii Arsenal”Kwa tamaduni zetu ni vibaya kumzungumzia vibaya Marehemu”

Chanzo: millardayo.com